Fahamuzaidimedia #Maoni ya wajumbe #Bungeni
Wananchi Watoa maoni kuhusu hoja ya mbunge mbunge kuwa posho, mishahara yao haitoishi.
Wakitoa maoni yao katika mtandao wa kijamii wa Instagram wa Mwananchi ulioweka habari hiyo na video ya mbunge huyo akieleza hali ngumu ya wabunge, baadhi ya watu hao wamemtaka mbunge huyo kuachana na kazi hiyo ya uwakilishi wa wananchi kama anaona haina maslahi.
Mbunge huyo aliyasema hayo Jumatatu Juni 21, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22, akiwataka wabunge wenzake kuwaambia ukweli wananchi.
Kauli hiyo imeungwa mkono na Tairo.Florianofficial akisema, “kawaida pesa haijawahi kutosha...,kwenu ndugu wananchi.”
Naye Emanuelyjaphet6790 amesema kauli hiyo ni dalili la ombwe la wabunge wa upinzani bungeni, “bila shaka tutajua umuhimu wa upinzani inawezekana tulikuwa hatuelewi hivi mtu analipwa milioni 12 na bado hazitoshi na mwalimu anayelipwa 400,000 asemeje? Du! Ama kweli.”
Wakati Jk_shoot_it akidai kuwa mshahara wa mbunge ni sawa na mtaji wa kijana mtaani, Nasra7162 amesema,“ndio tabu yakuchagua wabunge masikini, njaa ndio zinawapeleka bungeni wapo kuwaza mishahara na sio kutatua shida za wananchi waliowapigia kura.”
Je wewe maoni yako ni yapi ...? Toa maoni yako @Fahamu Zaidi media na usisahau ku subscribe YouTube channel yetu @Fahamu zaidi channel

COMMENTS