Msemaji mkuu wa mabingwa Mara nne Simba sport klabu usiku wa kuamkia leo amesema maneno mazito juu ya mtendaji mkuu wa timu hiyo bavbra Go...
Msemaji mkuu wa mabingwa Mara nne Simba sport klabu usiku wa kuamkia leo amesema maneno mazito juu ya mtendaji mkuu wa timu hiyo bavbra Gonzalez ambaye ameonekana kupishana nae siku za hivi karibu.Haji manara amezungumza kupitia ujumbe wa sauti alioutuma Instagram akitoa maneno ya kumlaani vibaya bavbra
"Yani unapenda kuongea vitu vya hovyo unapenda kunizaririsha kila siku kwann lakini bavbra" amesema manara kupitia voice note aloyoituma katika kurasa mbalimbali za Instagram
Manara amedai kuwa CEO huyo amekuwa akimuandama kila wakati na alitamani kuacha kazi kwa sababu yake yeye lakini alihairisha uamuzi huo mara baada ya mwenyekiti wa body Mohamed dewji kumtuliza
Manara aliongeza pia kuwa bavbra alimsingizia. Kuwa juzi alikwenda katika kambi ya yanga na kudai kuwa anahujumu timu
Manara alimaliza kwa kumuahidi CEO huyo kuwa aache kumtisha na Kama ataendelea Basi ataondoka katika klabu hiyo ya Simba
*MSIMBAZI* *KUMEKUCHA*

COMMENTS