Karibu Sana katika sports updates za fahamu zaidi channel leo ikiwa Ni ALHAMIS 21-Oct-2021 Tutaangazia tetesi za usajili barani ulaya ✍️k...
Karibu Sana katika sports updates za fahamu zaidi channel leo ikiwa Ni ALHAMIS 21-Oct-2021
Tutaangazia tetesi za usajili barani ulaya
✍️kwa mujibu wa mtandao wa Goal Mshambuliaji wa Argentina na Juventus Paul Dybala,27, anakaribia kusaini mkataba mpya wa muda mrefu kuendelea kuitumikia klabu yake ya Juventus.
lakini pia kwa mujibu wa sun Baada ya Newcastle kuachana na kocha wao Steve Bruce,Inaripotiwa Antonio Conte amekataa nafasi ya kuwa kocha mpya wa Newcastle na kuisubiri nafasi ya kuwa kocha mpya wa ManUtd kama itatokea hapo mbeleni
Orodha ya wagombea wa kuchukua nafasi ya Bruce huko Newcastle United sasa imebaki na Eddie Howe, Paulo Fonseca na Lucien Favre, ambao kila mmoja alifanya mazungumzo ya awali na klabu wiki iliyopita.
✍️Chelsea wako tayari kumfanya kiungo wa England Mason Mount,22, kuwa mmoja wa wanaolipwa kipato cha juu wakati klabu ikijiandaa kufungua mazungumzo ya mkataba mpya na mchezaji huyo.
✍️ Mshambuliaji wa Spain Ansu Fati, 18, anakaribia kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na Barcelona ambao utakua na Kifungu Cha kuachiliwa(Release Clause) cha €1B (£846M) sawa mwenzake Mhispania Pedri, 18.
✍️Beki wa kulia wa atletico Madrid na England Kieran Trippier, 31, ambaye alikuwa akihusishwa sana na kuhamia Man Utd msimu wa joto, amesema "angependa" kucheza kwenye Ligi ya EPL tena. (Mirror)
✍️Bosi wa ManUtd Ole Gunnar Solskjaer atatafuta kuondoa wachezaji wasiopungua watano kutoka kikosi chake wakati wa dirisha dogo la uhamisho litakapofunguliwa mnamo Januari. (Sun)
✍️Liverpool, Borussia Dortmund au RB Leipzig watalazimika kulipa kati ya €30M hadi €40M kumsaini mshambuliaji wa RB Salzburg na Ujerumani Karim Adeyemi, 19..(ORF -in Germany)
Wamiliki wapya wa Newcastle United bado hawajawasiliana na meneja Steve Bruce baada ya kipigo kutoka Tottenham Hotspur siku ya Jumapili wakiwa uwanja wa nyumbani. (Star) in
COMMENTS