Timu ya taifa ya ufaransa imeaga rasmi mashindano ya mataifa ya ulaya Mara baada ya kuondolewa na timu ya taifa ya Switzerland katika mch...
Timu ya taifa ya ufaransa imeaga rasmi mashindano ya mataifa ya ulaya Mara baada ya kuondolewa na timu ya taifa ya Switzerland katika mchezo ulioamuliwa kwa mikwaju ya penati Mara baada ya dakika 120 kuisha kwa sare ya 3_3.
Ufaransa ambao Ni mabingwa wa kombe la dunia 2018 walionekana kuzidiwa katika kipindi Cha kwanza Mara baada ya kuruhusu Gori dakika ya 15 kupitia kwa mchezaji wa Switzerland seferovic . lakini kipindi Cha pili wafaransa walirejea vyema na kurudisha gori na kusawazisha dk 57 kuptia kwa mchezaji wao karim Benzema ambaye pia dakika 2 mbele akaongeza bao la pili kabla ya Paul Pogba kuongeza bao la tatu dk 75 na kuufanya ubao usemeke 3_1 lakini magori hayo hayakudumu kwani Switzerland walianza kushambulia kwa Kasi na kufanikiwa kupata Gori la pili kupitia kwa mchezaji Seferovic dakika ya 81 na kuwafanya waongeze nguvu ya kushambulia na kusawazisha kabisa Gori la tatu kupitia kwa mchezaji Gavranovic katika dakika za majeruh (90). Licha ya kuongeza Dakika 30 lakini hazikuweza kubadilisha kabisa matokea Hadi mikwaju ya penati ilipoamua na kuisha kwa 4_5 Mara baada ya mbape kukosa mkwaju wa mwisho.
Written by Justine Cossan

COMMENTS