Simba na yanga zatakiwa kulipa faini milioni sita kwa kila timu huku mukoko na Morrison wakifungiwa kutocheza michezo mitatu klabu kubwa na...
Simba na yanga zatakiwa kulipa faini milioni sita kwa kila timu huku mukoko na Morrison wakifungiwa kutocheza michezo mitatu
klabu kubwa na kongwe Tanzania Simba na yanga leo hii zimepewa adhabu mbalimbali zikiwemo kiasi cha fedha milioni sita kwa kila timu kutokana na makosa mbalimbali waliyoyafanya wakati wa mchezo wa Fainali ya Azam sport Federation cup ulipofanyika jumapili ya mwezi julai tar 25 ambapo Simba aliibuka na ubingwa Mara baada ya kuifunga yanga Goli moja kwa Sifuri
Adhabu hizo zimetolewa na bodi ya ligi Tanzania TPBL kwa kuzingatia vifungu mbalimbali vya sheria vilivyovunjwa na timu hizo siku ya Fainali
Simba imepigwa faini ya milioni mbili kwa kosa la viongozi na mashabiki kulazimisha kuingia uwanjani wakati wa mazoezi maalumu ya timu hizo hali iliyopelekea uharibifu wa miundo mbinu huku mchezaji wao Bernad Morrison akipigwa faini ya million tatu na kufungiwa michezo mitatu katika timu hiyo kwa kosa la utovu wa nidhamu Mara baada ya kuvua bukta wakati wa mchezo huo lakini pia Simba imepigwa faini ya laki tano tano kwa makosa mawili yaloyosababishwa na utovu wa nidhamu kwa wachezaji wake likiwemo la kutofuata utaratibu wakati wa uvaaji wa medali katika mchezo huo
Huku yanga wakiadhibiwa kutokana na makosa mbalimbali Kama vile ,kosa la mukoko kumpiga bocco ambapo mchezaji huyo ameadhibiwa kutocheza michezo mitatu na faini ya laki tano lakini pia kipa farouk shikhalo na kocha nabi wapegwa faini ya laki tano tano kwa kila mmoja
Sanjali na hayo yanga pia imeadhibiwa faini ya shilingi million moja kwa kutofuata utaratibu wakati wa kuingia uwanjani kwa kuingilia mlango wa mashabiki huku adhabu nyingine Ni kosa la mashabiki kuwarushia chupa waaamuzi wa mchezo
Pamoja na makosa mengine yaliyopelekea kufikia kiasi cha Milioni sita kwa timu hiyo

COMMENTS