Mara baada ya mtanange mkali uliowakutanisha wababe wa VPL na watani wa jadi simba na yanga hapo jana na simba kupokea kichapo cha bao moja...
Mara baada ya mtanange mkali uliowakutanisha wababe wa VPL na watani wa jadi simba na yanga hapo jana na simba kupokea kichapo cha bao moja kwa bila
Sasa simba inatakiwa kuongeza jitiada katika michezo ijayo ili kuweza kunyakua ubingwa kwa mara ya nne mfululizo.endapo simba angeshinda dhidi ya mpinzani wake hapo jana rasmi angetangaza ubingwa kwani wangefikisha alama 76 ambazo yanga isingeweza kuzifikia lakini ushindi wa yanga unailazimu simba kushinda michezo mitatu ili kujihakikishia ubingwa. Simba hadi sasa ina alama 73 huku yanga akiwa nyuma akiwa na alama 70 licha ya simba kubakisha michezo minne ambayo ni dhidi ya KMC,COATAL UNION, AZAM na NAMUNGO bado wanatakiwa kufikisha alama 79 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote hapo ndipo watakuwa mabingwa
JE YANGA WANAWEZA KUPINDUA MEZA NA KUBEBA UBINGWA? Japo ni ngumu lakini inawezekana. Ikumbukwe hadi sasa yanga imesalia na michezo miwili tu na endapo itashinda yote itafikisha alama 76 hivyo ili yanga abebe ubingwa ni lazima simba apoteze michezo yote iliyosalia au apate sare michezo miwili na afungwe miwili

COMMENTS