AANDIKA KISA CHOTE MARA BAADA YA TUKIO LA DUBAI MWIJAKU"KULIPAKISASI NI KUPOTEZA MUDA" Dc Mwijaku Anaandika @mwijaku Watu hupiti...
AANDIKA KISA CHOTE MARA BAADA YA TUKIO LA DUBAI
MWIJAKU"KULIPAKISASI NI KUPOTEZA MUDA"
Dc Mwijaku
Anaandika @mwijaku
Watu hupitia maumivu ya kukataliwa na kusalitiwa. Lakini hii haimaanishi ndio mwisho wa maisha. Kuachwa au kuumizwa hakumaanishi ndio maisha hayawezi kuendelea au haiwezekani kuja kupenda tena.
Tunapotendewa hayo, tujifunze kusamehe kwani kwa kufanya hivyo tunatibu mioyo yetu na kuruhusu moyo kupokea yale yaliyo bora kwetu.
Kulipiza kisasi kwa wale waliotuumiza sio jambo la busara na hekima hata kidogo. Ni upotezaji muda. Ni kama kuamua kuwa mpumbavu kwa sababu ya mpumbavu mmoja asiejielewa aliyekufanyia upumbavu.
Muda mwingine lazima hekima itumike, unamsamehe mtu hata kama yeye binafsi hajakuomba msamaha, unamuacha aende, unabaki na amani yako na unaendelea na maisha.
Kwa kufanya hivyo hakukufanyi uonekane kama ni dhaifu, bali inaonyesha kwamba unathamini sana nafsi yako kuliko ujinga uliofanyiwa.
Tunapatikana Youtube kama Fahamuzaidi channel



COMMENTS